Jumatatu Marchi 05,2018 MTAKATIFU JOHN JOSEPH WA MSALABA

Mtakatifu John Joseph wa Msalaba Mtakatifu John Joseph alizaliwa mwaka 1654, katika kisiwa cha Ischia,karibu na Naples, Italia.Akiwa na miaka 16 tu, alijiunga na shirika la Wa Franciscan. Miaka 3 tu baadae ,alitumwa kwenda kuanzisha monasteri huko Piedmont. Baada ya kusoma, alipata daraja la upadri. Kwa idhini ya wakuu wake wa shirika, alijenga monasteri nyingine ambayo hata hivyo mwaka 1702 ,aliiacha, baada ya mgawanyiko wa majimbo, kati ya Italia na Hispania. Baada ya maangaiko, alifanikiwa kujenga manosteri nyingine ikiwa ni sehemu ya shirika lililobaki Hispania. Mtakatifu John Joseph alikufa mwaka 1734 March 5,huko Ischia, Naples Italia.Akatangazwa mwenye heri mwaka 1789 24 May na Papa Pius VI. Akatangazwa mtakatifu mwaka 1839 May 29 na Papa Gregory XVI.   Watakatifu wengine wa […]

Jumamosi Marchi 03,2018 MTAKATIFU KUNEGUNDA,MJANE

Mtakatifu Kunegunda, Mjane Mtakatifu Kunegunda, alikuwa Binti wa Siegfried, ambaye alikuwa mtawala wa Luxemburg. Alizaliwa mwaka 975. Aliolewa na mtakatifu Henry, ambaye alikuwa mtawala wa Bavaria .Lakini alikuwa ameweka nadhiri kuwa Bikira katika maisha yake yote. Na mume wake, alikubaliana na nadhiri hiyo.Mwaka 1014 ,mtakatifu Kunegunda alifuatana mume wake, walienda Roma.Huko Papa Benedict VIII, alimvika Henry taji ,kuwa mtawala wa dola ya Warumi. Lakini mtakatifu Kunegunda, alipata shutuma mbalimbali , lakini alimudu kuzimu tuhuma hizo, hata kutembea juu ya vipande ya chuma vikiwa moto.Na hakuungua . Alienda kwenye mafungo,huko Hesse, lakini aliugua sana.Akaweka nadhiri kujenga monasteri huko Kaffungen, karibu na Cassel katika jimbo la Paderborn. Alipopona, alitimiza ahadi yake , na kuikabidhi monasteri hiyo kwa watawa wa Benedictine. Mume wake, […]

Ijumaa Marchi 02,2018 WENYEHERI CHARLES MWEMA NA  HENRY  SUSO

Mwenyeheri Charles mwema  Mwenyeheri Henry Suso Mwenyeheri Charles mwema Mwenyeheri Charles alizaliwa mwaka 1083, huko Odence, Denmark. Alikuwa mwana wa mfalme Canute wa Denmark. Mwaka 1086 baba yake aliuwawa, na mama yake alimpeleka kulelewa na Robert ambaye alikuwa mtawala wa Flanders (Ubelgiji). Alipokuwa mkubwa aliandamana na Robert, akawa shujaa,na alishiriki vita vya msalaba. Baada ya kifo cha Robert, alitawala mwanae aliyeitwa Baldwin. Na baada ya kifo cha Baldwin, Charles alianza kutawala Flanders, mwaka 1119. Katika utawala wake, alipata maadui wengi matajiri. Kwa kuwa alizingatia haki kwa maskini, na kuondoa njia zote za ukandamizaji kwa watu wa chini.Alileta amani na maelewano, na kuhakikisha maskini wanapata chakula kwa bei nafuu. Baadhi ya watu walipanga kumuua, alipewa tahadhari juu ya mipango hiyo, lakini alimtegemea […]

Alhamisi  Marchi 01,2018 MTAKATIFU SUITBERT WA KAISERWEEDT,ASKOFU

Mtakatifu Suitbert wa Kaiserwerdt, Askofu Mtakatifu Suitbert, alizaliwa mwaka 647, huko Northumbria, Uingereza. Alisoma katika shule za Ireland pamoja na mtakatifu Egbert. Kulipotolewa ombi la kuhubiri katika Frisians (Ujerumani ) aliteuliwa mtakatifu Wigbert, ambaye hakufanikiwa sana . Mtakatifu Egbert alimtuma mtakatifu Willibrord ambaye alifuatana na wenzake 12, akiwemo Mtakatifu Suitbert. Walisafiri mpaka Rhine ,na wakaenda kuweka makao yao Utrecht (Ujerumani ).Wamisionari hao wapya walifanya kazi kwa mafanikio makubwa, wakisaidiwa na mmoja wa watawala aliyeitwa Pepin. Mtakatifu Suitbert alirudi Uingereza na mwaka 693,aliteuliwa kuwa Askofu mmisionari wa Frisia.Akaweka makao makuu yake Kaiserwerdt. Akafanya kazi za Mungu kwa mafanikio makubwa, japo baadae nchi ilitawaliwa na wapagani. Mtakatifu Suitbert alirudi katika mji wa Rhine, katika kisiwa kidogo, karibu na Düsseldorf, palipoitwa Suitbert -Insel […]

Jumatano februari 28,2018 WATAKATIFU  ROMANUS ABATE, NA LUPICINUS

Mtakatifu Romanus Abate Mtakatifu Romanus alizaliwa huko Upper Bugey Ufaransa. Akiwa na miaka 35, aliamua kwenda kuishi upweke, akisali na kuomba,katika eneo la Condat .Watu wengine, akiwemo mdogo wake (Mtakatifu Lupicinus ) walijiunga nae,na akawa kiongozi wao.Watakatifu Romanus na Lupicinus, walijenga na kuanzisha monasteri kadhaa, ikiwemo Condat, Lauconne, La Balme , na Romainmôtier huko Switzerland. Mtakatifu Romanus, alipata pia daraja la upadri mwaka 444, alipewa na mtakatifu Hilary (Askofu wa Arles ). Mtakatifu Romanus alikufa mwaka 460, Februari 28 na kuzikwa katika manosteri ya La Beaume, Ufaransa. Mtakatifu Lupicinus Mtakatifu Lupicinus, alikuwa ni mdogo wa Mtakatifu Romanus. Aliungana na kaka yake katika utawa. Ndugu hawa, walishirikiana kuanzisha manosteri kadhaa, na walitumia muda wao kusali, na kujifunza maandiko matakatifu. Mtakatifu Lupicinus […]

Jumanne februari 27,2018 WATAKATIFU LEANDER,ASKOFU WA SEVILLE  NA GABRIEL WA MAMA YETU WA MATESO

Watakatifu Leander Askofu na Gabriel  wa Mama yetu wa Mateso Mtakatifu Leander, alizaliwa mwaka 534, huko Cartagena, Spain.Alianza kwa kuwa mtawa wa kwanza wa shirika la Benedictine hapo Seville, na baadae kupata daraja, na kuwa Askofu wa Seville mwaka 579. Kutokana na kazi zake na msimamo wake, alipelekwa uhamishoni huko Constantinople. Huko alikutana na mwakilishi wa Papa,ambaye walitokea kuwa marafiki wakubwa.Balozi huyo baadae alikuwa Papa Gregory mkuu. Mtakatifu Leander, aliandika vitabu, na kufanya mafundisho sehemu mbalimbali . Aliporudi Seville, aliendelea na mafundisho yake, hata kuwaokoa wenye mafundisho ya wapinga Kristo. Mtakatifu Leander Askofu, alikufa mwaka 600. Mtakatifu Gabriel wa Mama yetu wa Mateso Mtakatifu Gabriel, alizaliwa mwaka 1838 ,March 1 , huko Assisi Italia, na akabatizwa na kuitwa Francis Possenti. […]

Jumatatu februari 26,2018 MTAKATIFU PORPHYRY,ASKOFU

Mtakatifu Porphyry, Askofu Mtakatifu Porphyry (Profiri) ,alizaliwa mwaka 347 huko Thessalonika, Macedonia, katika familia njema ya kigiriki. Akiwa na miaka 25, aliamua kwenda kukaa peke yake, kando ya mto Jordan, huko Palestina na baadae Jerusalem. Aligawa urithi wake, na akafanya kazi ya kutengeneza viatu. Baadae alipata sacramenti ya Upadri. Mwaka 396, aliteuliwa kuwa Askofu wa Gaza.Akiwa Askofu, alikumbana na tatizo la wapagani, lakini aliweza kuwafanya kuelewa neno la Mungu. Aliweza kujenga kanisa, katika eneo lenye wapagani wengi, ikiwa ni ishara ya kufanikiwa kwake, katika uinjilishaji. Mtakatifu Porphyry alikufa mwaka mwaka 420, Februari 26.   Watakatifu wengine wa leo ni Mt. Isabel wa France Mt. Alexander Mt. Alexander wa Alexandria Mt. Dionysius wa Augsburg Mt. Faustinian Mt. Papias Mt. Victor

Jumamosi februari 24,2018 MTAKATIFU  MONTANUS NA WENZAKE MASHAHIDI

Mtakatifu Montanus na wenzake mashahidi Mtakatifu Montanus na wenzake,Julian,Lucius,Victorius (Padre) Mtakatifu Flavian, pamoja na wengine watano, walizaliwa katika mji wa Carthage (Tunisia) Mwaka 259 kulikuwa na uasi katika Carthage, na nyakati hizo ikiwa chini ya mtawala mpinga Kristo, Valerian. Mwangalizi wa mji, alipeleka lawama zote kwa Wakristo, na akaanza kuwakamata. Baada ya mateso makali , watakatifu hao waliuwawa kwa kukatwa vichwa mwaka huo wa 259.   Watakatifu wengine wa leo ni Mt. John Theristus Mt. Adela Mt. Betto Mt. Modestus Mt. Primitiva Mt. Sergius M/h. Tommaso Maria Fusco

Ijumaa februari 23,2018 MTAKATIFU POLYCARP,ASKOFU NA SHAHIDI

Mtakatifu Polycarp, Askofu na Shahidi Mtakatifu Polycarp alikuwa Askofu wa Smyrna (Uturuki ), na alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Mtakatifu Yohane, Mtume. Mtakatifu Polycarp, aliweza kusaidia maelewano kati ya wakristo, hasa alipoweza kutatua tatizo la nyakati za sikukuu ya Pasaka, katika makundi yaliyokuwa hayafuati kalenda ya Roma.Aliweza kuwarudisha wote, kusheherekea sikukuu ya Pasaka pamoja. Alipingana na wapinga Kristo bila woga, jambo lililosababisha kukamatwa kwake.Alipata maono yaliyomwonesha namna ya kifo chake kitakavyokuwa.Alijua kuwa angechomwa moto. Mtakatifu Polycarp aliuwawa kwa kuchomwa moto , kwa kutetea imani yake, huko Smyrna ,mwaka 156 Februari 23   Watakatifu wengine wa leo ni Mt. Alexander Akimetes Mt. Boswell Mt. Cerneuf M/h. Daniel Brottier Mt. Dositheus Mt. Felix wa Brescia Mt. Florentius M/h. Josephine Vannini Mt. Jurmin […]

Alhamisi februari 22,2018 MTAKATIFU PETRO,MTUME

Mtakatifu Petro, Mtume Ukuu wa Mtakatifu Petro, Mtume Leo tunawakumbuka jinsi Mtume Petro, alivyopewa ukuu wa kanisa. Sote tunajua Mtume Petro, alivyokuwa na Bwana wetu Yesu Kristo. Lakini katika Injili ya Mathayo 16:13-19, tunaona jinsi Mtume Petro, anavyojibu swali, ambalo Bwana, aliwauliza wanafunzi wake. Na tunaona baada ya kujibu, jinsi Bwana, alivyomwambia Petro, ufahamu na jibu la swali lake, vilitoka kwa Mungu Baba , mbinguni. Kisha tunaona jinsi Mtume Petro, anavyokabidhiwa kazi ya kulichunga na kulisimamia kanisa la Bwana Yesu Kristo. Hivyo Ukuu wa Petro Mtume, aliopewa na Bwana Yesu, unamfanya kuwa Papa wa kwanza wa kanisa ,mwenye mamlaka ya kufunga na kufungua lolote. Tumuombee Papa, Maaskofu na Mapadre, na wote wenye daraja katika kutekeleza majukumu yao, ili kanisa la […]