MASOMO YA MISA,MEI 09, 2018 JUMA LA SITA LA PASAKA, JUMATANO

SOMO 1 Mdo, 17: 15, 22-18:1 Hotuba ya Paulo mbele ya Arcopago. Somo katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Siku zile, wale waliomsindikiza Paulo wakampe. leka mpaka Athene; nao wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kwamba wasi- kawie kumfuata, wakaenda zao, Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini. Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, kwa Mungu asiyejulikana. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa […]

MASOMO YA MISA,MEI 08, 2018 JUMA LA SITA LA PASAKA, JUMANNE

SOMO 1 Mdo. 16 : 22-34 Paulo na Sila wanafungwa na kufunguliwa kwa mwujiza. Somo katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Siku ile, pale Filipi, wenyeji waliwakamata Paulo na Sila, wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, waka- watupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Naye akiisha kupata amri hii aka- watupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyi- mbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vika- legezwa. Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona […]

MASOMO YA MISA,MEI 07, 2018 JUMA LA SITA LA PASAKA, JUMATATU

SOMO 1 Mdo. 16 : 11-15 Paulo na wenzake (Sila na Timotheo) wanafika Filipi. Somo katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Tuling’oa nanga kutoka Troa, tukafika Samoth- rake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli; na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyo- nenwa na Paulo. Hata alipokwisha kubatizwa, […]

MASOMO YA MISA, MEI 06, 2018 DOMINIKA YA SITA YA PASAKA.

  SOMO 1 Mdo. 10 : 25-265 34-35, 44.48 Somo hili laonyesha maongozi ya Mungu juu ya wokovu wa watu wapagani. Akiongozwa na mwanga wa Roho Mtakatifu, Mtume Petro alitambua kwamba Wapagani haikuwapasa kutahiriwa ili waweze kuokoka kama Sheria ya Kiyahudi ilivyodai. Kwa upande wao imetakiwa tu wasadiki mafundisho ya Yesu na kupokea ubatizo. Somo katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Petro alipokuwa akiingia Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia. Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu. Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo, bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno, Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, […]

MASOMO YA MISA,MEI 05, 2018 JUMA LA TANO LA PASAKA, JUMAMOSI

SOMO 1 Mdo. 16 : 1-10 Paulo na Sila wanamchukua Timotheo huko Listra na wanavuka Asia Ndogo kuhubiri. Somo katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Siku zile, Paulo alifika Derbe na Listra na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Myunani. Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio. Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamta- hiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani. Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, waka- wapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike. Makanisa yakatiwa nguvu katika ile Imani, hesabu yao ikaongezeka kila siku. Wakapita katika nchi ya Frigia […]

MASOMO YA MISA,MEI 04, 2018 JUMA LA TANO LA PASAKA, IJUMAA

SOMO 1 Mdo. 15 : 22-31 Hati ya mtaguso wa mitume huko Yerusalemu. Somo katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Siku zile, baada ya Mtaguso wa Yerusalemu, ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa Barnaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na kupeleka kwa mikono yao, Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu. Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbua kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, ambao Sisi hatukuwaagiza; Sisi tumeona vema, hali tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na […]

MASOMO YA MISA,MEI 03, 2018 JUMA LA TANO LA PASAKA, ALHAMIS

WATAKATIFU FILIPO NA YAKOBO MITUME SOMO 1 1 Kor. 15:1-8 Kristu alimtokea Yakobo, kisha akawatokea mitume wote. Somo katika waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Wakorintho .Ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri; isipokuwa mliamini ‘bure. Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo Yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenaVY0 maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwaalifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandikona ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thena- shara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hatasasa, ila baadhi yao wamelala; baadaye akamtokea Yakobo, tena na mitume wote;a […]

MASOMO YA MISA,MEI 02, 2018 JUMA LA TANO LA PASAKA, JUMATANO

SOMO 1 Mdo. 15 : 1-6 Mabishano kuhusu kutahiriwa, na mtaguso wa kwanza wa Mitume. Somo katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Siku zile, walishuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipota- hiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka. Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na wa- tu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo. Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana. Walipofika Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao. Lakini baadhi ya madhehebu […]

MASOMO YA MISA,MEI 01, 2018 JUMA LA TANO LA PASAKA, JUMANNE

MT. YOSEFU, MFANYAKAZI SOMO 1 Mwa. 1 : 26-2 : 3 Mwijaze nchi na kuitiisha. Somo katika kitabu cha Mwanzo. Mungu alisema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu; kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitamba- acho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwana- mume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawa- barikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu aka- sema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda […]

MASOMO YA MISA,APRIL 30, 2018 JUMA LA TANO LA PASAKA, JUMATATU

SOMO 1 Mdo. 14 : 5-18 Paulo na Barnaba wanahubiri Likaonia, na wanamponya kiwete. Somo katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Siku zile, palipotokea shambulio la watu wa Mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga kwa mawe, wao wakapata habari wakakimbilia Listra na Derbe, mji wa Likaonia, na nchi zilizo kando kando; waka- kaa huko, wakiihubiri Injili. Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mamaye, ambaye hajaenda kabisa. Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; ambaye akamkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa, akasema kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawasawa. Akasimama upesi akaenda. Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wa- kapaza sauti zao, wakisema […]