HIJA YA WANA-TMCS-DIT KATIKA KITUO CHA HIJA PUGU.

TUMSIFU YESU KRISTO. Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uzima. Leo Jumamosi tarehe 9 June 2018 wana TMCS-DIT tunafanya Hija katika kituo cha Hija Pugu. Hapa tunajifunza mambo mbalimbali ikiwemo Biblia ya Ardhini, Kutembelea Makaburi ya Wamisionari, Kutembelea Kaburi liliondaliwa kwa ajili ya Mwadhama Polycarp Cardinali Pengo, Kuona Nakala ya Sanda halisi ya Yesu, Kufanya Njia ya Msalaba na mambo mengine mengi yanaayohusu Kanisa Katoliki na imani kwa ujumla. Katika Hija hii tumeambatana na Walimu wetu walezi ambao ni  Dr. Lugumila na Mr. Muhale.           Tafakari hii inatukumbusha kuwa tayari kila wakati kwani duniani tunapita tu na siku moja nasi tutarudi mavumbini.          

MATENDO YA HURUMA 2 JUNE 2018

Tumsifu Yesu Kristo. “TMCS-DIT KIPAOMBELE KWA WAHITAJI”. Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Uzima na Afya njema. Tukiongozwa na Kauli Mbiu yetu “TMCS-DIT KIPAOMBELE KWA WAHITAJI”, Leo tarehe 2 June 2018, TMCS-DIT tunatembelea Kituo cha Watoto cha Mt. Theresa, NYUMBA YA AMANI NA FURAHA kilichopo Mburahati Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya MATENDO YA HURUMA. Hapa tunashiriki shughuli mbalimbali pamoja na Watoto ikiwemo Usafi, Michezo, Sala pamoja na Nyimbo. Pia tutawasilisha mahitaji mbalimbali kwa ajili ya Watoto. Tunashukuru Uongozi wa Kituo cha Mt. Theresa kwa kutupatia nafasi ya kushiriki  na Watoto siku ya leo. MUNGU AWABARIKI.  Imeandaliwa na TEHAMA TMCS-DIT.  Source: Google Map.   Kituo cha Watoto cha Mt. Theresa, NYUMBA YA AMANI NA FURAHA kilichopo Mburahati […]

TMCS-DIT MAHAFALI 2018 TMCS-DIT tunamshukuru Mungu kwa siku hii ya pekee tunapowapongeza wanafunzi wenzetu wanaohitimu katika ngazi za shahada na stashahada.Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya hawa wenzetu ambao tumekuwa nao pamoja katika kumsifu na kumtukuza Mungu kwa kipindi chote walichokuwa nasi. Siku hii inapambwa kwa matukio mbalimbali ikiwemo Ibada ya Misa Takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Bethania House Upanga na baadae tafrija fupi inayoendelea katika Hoteli ya Valentino Kariakoo. Wahitimu TMCS-DIT 2017/2018 wakiwa katika picha ya pamoja na Padre Mlezi Baba Luxford Lugongo baada ya Ibada ya Misa Takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Bethania House Upanga. Picha na TEHAMA TMCS-DIT. Mc .Fat Ros kutoka Chuo cha Uhasibu TIA akifanya kazi yake kwa ufaninisi mkubwa kuhakikisha kila mmoja anapata burudani.Baadhi ya […]