MASOMO YA MISA,MEI 07, 2018 JUMA LA SITA LA PASAKA, JUMATATU

MASOMO YA MISA,MEI 07, 2018 JUMA LA SITA LA PASAKA, JUMATATU

SOMO 1
Mdo. 16 : 11-15
Paulo na wenzake (Sila na Timotheo) wanafika Filipi.

Somo katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

Tuling’oa nanga kutoka Troa, tukafika Samoth- rake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli; na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyo- nenwa na Paulo. Hata alipokwisha kubatizwa, Yeye na nyumha yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatushurutisha.
Neno la Bwana.

 

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 149 : 16, 9 (K) 4

l. Aleluya.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Sifa zakc katika kusanyiko la watauwa.
Israeli na amfurahie Y eye aliyemfanya,
Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.
(K) Bwana awaridhia watu wake.
au: Aleluya.

2.Na walisifu jina lake kwa kuchcza,
Kwa matari na kinubi wamwimbie.
Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake,
Huwapamba wenye upole kwa wokovu. (K)
3. Watauwa na waushangilie utukufu,
Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,
Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wote. (K)

 

SHANGILIO
Rum. 6 : 9

Aleluya, aleluya,
Kristo akiisha kufufuka katika wafu
hafi tena wala mauti haimtawali tena.
Aleluya.

 

INJILI
Yn. 15 : 26 – 16:4

Roho wa Kweli ajapo, atamshuhudia Yesu Kristo.

Somo katika Injili ilivyoandikwa na Yohane.

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: A japo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishu- hudia. Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami. Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja ata- kapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia.
Neno la Bwana.