HIJA YA WANA-TMCS-DIT KATIKA KITUO CHA HIJA PUGU.

HIJA YA WANA-TMCS-DIT KATIKA KITUO CHA HIJA PUGU.

TUMSIFU YESU KRISTO. Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uzima.

Leo Jumamosi tarehe 9 June 2018 wana TMCS-DIT tunafanya Hija katika kituo cha Hija Pugu. Hapa tunajifunza mambo mbalimbali ikiwemo Biblia ya Ardhini, Kutembelea Makaburi ya Wamisionari, Kutembelea Kaburi liliondaliwa kwa ajili ya Mwadhama Polycarp Cardinali Pengo, Kuona Nakala ya Sanda halisi ya Yesu, Kufanya Njia ya Msalaba na mambo mengine mengi yanaayohusu Kanisa Katoliki na imani kwa ujumla.

Katika Hija hii tumeambatana na Walimu wetu walezi ambao ni  Dr. Lugumila na Mr. Muhale.

 

Maelezo kutoka kwa Mwalimu  mstaafu wa Idara ya Maabara  Mr. Muhale ambaye pia ni Mlezi wetu.

 

 

Katika Ibada ya Njia ya Msalaba

 

 

ULIVYO WEWE NDIVYO TULIVYOKUWA SISI, NA TULIVYO SISI NDIVYO UTAKAVYOKUWA WEWE”

Tafakari hii inatukumbusha kuwa tayari kila wakati kwani duniani tunapita tu na siku moja nasi tutarudi mavumbini.

 

 

 

 

 

Makaburi ya Mapadre waasisi na walitoumikia Parokia ya Pugu